Vijana ni taifa la kesho,ni msemo wa wahenga,bila shaka wengi wetu tunaufahamu msemo huu.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tabia ya kuwaona vijana kama wasumbufu,watu wasiojielewa na mengine kama hayo,sikatai kwasababu kila familia ina misingi na taratibu zake katika malezi,na malezi hayohayo ndio leo yaliyo tuletea viongozi wala rushwa,mafisadi na wengine wengi wa aina hizo.
Lengo hapa nikuweka sawa baadhi ya mambo,japo kwa uelewa wangu tabia ni kama ngozi huwezi kuibadili,mfano katika jumuia yangu,vijana wenzangu kuna wenye mawazo ambayo hata mtoto wa primary hawezi kuyaleta mbele ya rafiki zake,mnapanga kusaidiana kutatua changamoto zinazowakabili,mnaandaa kikundi mkisajili ili muweze kudhaminiana katika mambo ya mikopo na biashara,mtu mzima(18+) analeta dharau na ujinga,anawafelisha.
Pamoja na mapungufu yetu lakini kuna vijana wanaojielewa,vijana ambao wana malengo na mipanga yao,ambao wako tayari kufanya kazi na vijana wenzao kujiletea maendeleo na taifa kwa ujumla.Katika maisha watu wa rika zote wana umuhimu,vijana ndio nguvu kazi ya taifa na wazee watupe uzoefu wao ili kazi zetu ziwe na tija,kwetu kama vijana na taifa kwa ujumla.
Vijana wapo katika sekta nyingi,kuna walio katika serikali,sekta binafsi ei mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na sie tulio katika sekta isio rasmi,walio serikalini i.e. watumishi wa umma wanajukumu la kuwa hudumia wananchi wote bila kusahau kutetea haki za vijana wenzao walio katika sekta zingine,ie sekta binafsi na isio rasmi
Vilevile vijana wa sekta binafsi na isio rasmi tuna wajibu wa kudai haki zetu,lakini hatuwezi kupata haki hizo bila ya kuwa na utaratibu,utaratibu wenyewe ni kujiunga katika vikundi,tuvisajili ili tuweze kudhaminiana wenyewe kwa wenyewe.
Tuelimishane juu ya ile 5% ya vijana katika kila halmashauri,ni yetu,ila ili tuipate tujikusanye vijana tunaofahamiana vizuri,tuunde vikundi,tuvisajili,mwisho wa siku tuweze kudhaminiana wenyewe kwenye suala zima la mikopo.,,
Katika maisha ya kila siku,watu huwa tunajifunza mambo mbalimbali,tulipokosea jana,leo tunajirekebisha. Maisha ni safari,na katika safari hio kuna mambo mengi mapya tunakutana nayo,pia zipo changamoto mbalimbali tunakutana nazo,.....usikate tamaa,changamoto ziwe chachu ya kusonga mbele. Tupambane,kijana unapo tafuta maisha jaribu kuishi maisha yako,tamani mafanikio ya fulani,lakini usiishi kama fulani.
Comments
Post a Comment