Ujangili ni tatizo kubwa katika bara la afrika,ujangili umepunguza idadi ya wanyama pori
Serikali za nchi za afrika zimekuwa zikitumia njia mbalimbali katika kukabiliana na janga la ujangili,ie ushirikishwaji wa wananchi waishio kandokando ya hifadhi za wanyama pori,utungaji na ufuatiliaji wa sheria ndogondogo nk.
Mtanzania na mwafrika mwenzangu,wanyama pori ni rasilimali muhimu sana na urithi wetu tulioachiwa na mababu zetu,hata sisi tunajukumu la kulinda na kuendeleza mambo yote yahusuyo wanyama pori na mazingira yao kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae.
Mimi napinga ujangili,naunga mkono juhudi za serikali na mashirika mbalimbali katika vita dhiidi ya ujangili.
Penda nchi yako,penda afrika yako,wapende wanyama pori wetu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadae.SEMA HAPANA KWA UJANGILI
Habari,mwanangu aisha ni blog ya kijamii inayokupatia habari mbalimbali zinazo husu mazingira yetu,ie mazingira ni kila kinachomzunguuka mwanadamu Lengo kuu la blog hii ni kupashana habari juu ya mambo yanayotuzunguka,maoni yako yanamchango mkubwa sana,ila tafadhari,tumia lugha nzuri kwani blog hii ni ya watu wo te
Comments
Post a Comment