Vijana ni taifa la kesho,ni msemo wa wahenga,bila shaka wengi wetu tunaufahamu msemo huu. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tabia ya kuwaona vijana kama wasumbufu,watu wasiojielewa na mengine kama hayo,sikatai kwasababu kila familia ina misingi na taratibu zake katika malezi,na malezi hayohayo ndio leo yaliyo tuletea viongozi wala rushwa,mafisadi na wengine wengi wa aina hizo. Lengo hapa nikuweka sawa baadhi ya mambo,japo kwa uelewa wangu tabia ni kama ngozi huwezi kuibadili,mfano katika jumuia yangu,vijana wenzangu kuna wenye mawazo ambayo hata mtoto wa primary hawezi kuyaleta mbele ya rafiki zake,mnapanga kusaidiana kutatua changamoto zinazowakabili,mnaandaa kikundi mkisajili ili muweze kudhaminiana katika mambo ya mikopo na biashara,mtu mzima(18+) analeta dharau na ujinga,anawafelisha. Pamoja na mapungufu yetu lakini kuna vijana wanaojielewa,vijana ambao wa...