Skip to main content

Tabata reli

     Vijana ni taifa la kesho,ni msemo wa wahenga,bila shaka wengi wetu tunaufahamu msemo huu.
      Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tabia ya kuwaona vijana kama wasumbufu,watu wasiojielewa na mengine kama hayo,sikatai kwasababu kila familia ina misingi na taratibu zake katika malezi,na malezi hayohayo ndio leo yaliyo tuletea viongozi wala rushwa,mafisadi na wengine wengi wa aina hizo.
      Lengo hapa nikuweka sawa baadhi ya mambo,japo kwa uelewa wangu tabia ni kama ngozi huwezi kuibadili,mfano katika jumuia yangu,vijana wenzangu kuna wenye mawazo ambayo hata mtoto wa primary hawezi kuyaleta mbele ya rafiki zake,mnapanga kusaidiana kutatua changamoto zinazowakabili,mnaandaa kikundi mkisajili ili muweze kudhaminiana katika mambo ya mikopo na biashara,mtu mzima(18+) analeta dharau na ujinga,anawafelisha.
      Pamoja na mapungufu yetu lakini kuna vijana wanaojielewa,vijana ambao wana malengo na mipanga yao,ambao wako tayari kufanya kazi na vijana wenzao kujiletea maendeleo na taifa kwa ujumla.Katika maisha watu wa rika zote wana umuhimu,vijana ndio nguvu kazi ya taifa na wazee watupe uzoefu wao ili kazi zetu ziwe na tija,kwetu kama vijana na taifa kwa ujumla.
     Vijana wapo katika sekta nyingi,kuna walio katika serikali,sekta binafsi ei mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na sie tulio katika sekta isio rasmi,walio serikalini i.e. watumishi wa umma wanajukumu la kuwa hudumia wananchi wote bila kusahau kutetea haki za vijana wenzao walio katika sekta zingine,ie sekta binafsi na isio rasmi
      Vilevile vijana wa sekta binafsi na isio rasmi tuna wajibu wa kudai haki zetu,lakini hatuwezi kupata haki hizo bila ya kuwa na utaratibu,utaratibu wenyewe ni kujiunga katika vikundi,tuvisajili ili tuweze kudhaminiana wenyewe kwa wenyewe.
      Tuelimishane juu ya ile 5% ya vijana katika kila halmashauri,ni yetu,ila ili tuipate tujikusanye vijana tunaofahamiana vizuri,tuunde vikundi,tuvisajili,mwisho wa siku tuweze kudhaminiana wenyewe kwenye suala zima la mikopo.,,
    

Comments

Popular posts from this blog

Wild life

     Hi every body,it's wednesday again,let's talk a little bit about african wild life       Africa we have a vast range of wild life that cannot found anywhere in the world,different species of animals and trees,from the innocent gazel to the big fives       These animals together with their sorroundings needs our support so as can provide us with the maxmum benefits       Our wildlife contribute alot to our social economy activities,i.e our nations get alot of money from tourism,and that money goes either directly or indirect to our societies,like schools for the kids,hospitals and other development projects like roads,water supplies, etc      We need to join our efforts,to protect,defend and conserve our wildlife for us and the future generation,everybody in his/her position,leaders and the societies in general,together we can can make the changes we want,love your country,conserve our wildlife

JAMII ZETU

  Katika maisha ya kila siku,watu huwa tunajifunza mambo mbalimbali,tulipokosea jana,leo tunajirekebisha.   Maisha ni safari,na katika safari hio kuna mambo mengi mapya tunakutana nayo,pia zipo changamoto mbalimbali tunakutana nazo,.....usikate tamaa,changamoto ziwe chachu ya kusonga mbele.   Tupambane,kijana unapo tafuta maisha jaribu kuishi maisha yako,tamani mafanikio ya fulani,lakini usiishi kama fulani.

Karibu katika blog yako mtanzania

Habari,mwanangu aisha ni blog ya kijamii inayokupatia habari mbalimbali zinazo husu mazingira yetu,ie mazingira ni kila kinachomzunguuka mwanadamu Lengo kuu la blog hii ni kupashana habari juu ya mambo yanayotuzunguka,maoni yako yanamchango mkubwa sana,ila tafadhari,tumia lugha nzuri kwani blog hii ni ya watu wo te